Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC waisaka nafasi ya Simba Kimataifa, waichapa KMC bao 2

IMG 0264.jpeg Azam FC waisaka nafasi ya Simba Kimataifa, waichapa KMC bao 2

Mon, 13 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Azam FC usiku wa jana iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na kiungo Mkongo, Yannick Bangala dakika ya 11 na winga Mgambia, Jibril Sillah dakika ya 37, wakati bao pekee la KMC limefungwa na mshambuliaji mzawa, Waziri Junior dakika ya 15.

Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 60 katika mchezo wa 27, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nane na mabingwa watetezi, Yanga SC ambao pia wana mechi moja mkononi.

Kwa upande wao KMC baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 33 za mechi 27 pia nafasi ya sita.

Ikumbukwe kuwa Msindi wa Ligi na timu inayokamata nafasi ya pili zinakwenda kuiwakilisha nchi katika Michuano ya CAF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live