Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC waifata Al Akhdar

271A2848 1170x650 Azam FC

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha wachezaji 25 wa Azam FC kinataraji kuondoka leo Alhamisi ya Oktoba 6,2022 kimesafiri kuelekea jijini Benghazi, nchini Libya majira ya Saa 11.25 Alfajiri kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika 2022-2023..

Miongoni mwa nyota 25 wanaosafiri kuelekea Libya ni pamoja na Ali Ahmada,Lusajo Mwaikenda,Bruce Kangwa, James Akaminko,Sospeter Bayana,Aggrey Morris,Iddi Nado na Yahya Zayd.

Azam FC wataikabili klabu ya Al Akhdar ya Libya mnamo Oktoba 08-2022 siku ya Jumamosi majira ya Saa 2:00 Usiku huku nyota 7 wakiwemo  Wilbol Maseke,Kenneth Muguna,Ibrahim Ajib ,Ismail Aziz Kader,Shaaban Idd Chilunda na Rodgers Kola wakiachwa kwenye safari hiyo kutokana na sababu mbalimbali zinazowakabili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live