Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC wabanwa mbavu na Mashujaa Uwanja wa Chamazi

IMG 6788.jpeg Azam FC wabanwa mbavu na Mashujaa Uwanja wa Chamaz

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Azam FC wamelazimishwa sare ya bila mabao na Mashujaa katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku wa Jana Aprili 17 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 51 katika mchezo wa 23 na inabaki nafasi ya pili ikizidwa pointi nne na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi mbili mkononi.

Kwa upande wao Mashujaa FC ya Kigoma baada ya sare ya leo wanafikisha pointi 22 katika mchezo wa 23 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16 ikiizidi tu wastani wa mabao Tabora United waliyopanda Ligi Kuu msimu huu pamoja na JKT Tanzania.

Kwa ujumla hali si shwari kwa timu zote zilizopanda msimu huu, kwani JKT Tanzania nayo inashika nafasi ya 13 ikiwa na pointi 22 pia za mechi 22, wakati mabingwa mara mbili mfululizo, 1999 na 2000, Mtibwa Sugar wanashika mkia wakiwa na pointi 17 za mechi 22.

Ikumbukwe timu mbili za mwisho zitashuka Daraja mwisho wa msimu na mbili zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: