Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC wa moto sana, waishusha Simba kileleni

IMG 5503.jpeg Azam wanaongoza Msimamo wa Ligi Kuu Bara

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Azam FC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tanzania Prisons usiku wa Jumatatu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 11 na wazawa Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 47 na Nathaniel Chilambo dakika ya 82, wakati la Prisons limefungwa na Zabona Khamis dakika ya 90 na ushei.

Kwa ushindi huo, Azam FC wanafikisha pointi sita sawa na Simba, lakini wanakaa kileleni kwa wastani mzuri wa mabao, wakati Prisons inabaki na pointi yake moja baada ya wote kucheza mechi mbili mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: