Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC na mikakati mipya

Amin Popat 123 Azam FC na mikakati mipya

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa klabu ya Azam FC ‘Wanalamba lamba’ umesema, watahakikisha msimu ujao wa mwaka 2023-24 wanafanikiwa kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa kwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ ameiambia EATV kuwa, mpaka sasa wameshajihakikishia nafasi ya ushiriki wa kombe la shirikisho barani Afrika hivyo wanaendelea kuweka mipango ya kuboresha benchi la Ufundi na wachezaji.

"Tumeanza maandalizi mapema ya kuhakikisha tufanya vyema katika msimu ujao kwahiyo wapenzi wa Azam watarajiwa mambo mazuri kwa timu yao'' amesema Abdulkarim Amin ‘Popat’

Afisa Mtendaji huyo, amekiri kuwa, msimu huu wa mwaka 2022-23 wameshindwa kufikia malengo yao ya kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu NBC Tanzania na badala yake wameelekezea nguvu kubwa kutaka kubeba Ubingwa wa kombe la Shirikisho la Azam.

Azam FC ipo nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC Tanzania na alama 53 baada ya michezo 27 huku ikiwa nusu fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Simba SC mchezo utakaochezwa Mei 6, 2023 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live