Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC mambo yazidi kuwanyookea

Azam Namungo Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao lao la ushindi

Mon, 21 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam FC yaendeleza wimbi la ushindi hapo jana walipokuwa wageni wa Namungo ya Lindi baada ya kuitwanga kwa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa Novemba 20 majira ya saa 1:00 jioni katika uwanja wa Majaliwa.

Dakika ya 29 tu Azam ilikuwa imeshajipatia bao kupitia kwa beki wao Edward Manyama na ndilo bao ambalo lilisalia mpaka kumalizika kwa mchezo huo huku Namungo wakipoteza mchezo wao wa tatu mfululizo.

Azam FC ya ambayo ipo chini ya Kally Ongala inaendeleza makali yake ya kujipatia ushindi mnono kwa kila mechi ambazo inakabiliana nazo huku ikiwa ni mechi ya sita kushinda.

Namungo walipata adhabu ya kadi nyekundu kipindi cha pili na kufanya kucheza wakiwa pungufu huku wakijaribu kutafuta bao la kusawazisha lakini milango ikawa migumu huku mlinda mlango wa Wanalamba lamba akiwa na ubora wa hali ya juu.

Baada ya ushindi huo matajiri hao wa Chamazi wakipaa hadi kileleni wakipanda hadi nfasi ya kwanza kwenye msimamo na pointi zao 29 huku Namungo wao wakisalia katika nafasi ya 8 baada ya kupoteza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live