Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC kuzindua jezi, jengo jipya leo

Feisal Azam VzO.jpeg Azam FC kuzindua jezi, jengo jipya leo

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam FC imemtangaza Tabia Maulid Mwita Waziri wa wa Habari, Utamaduni na michezo kuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa jezi mpya za msimu wa 2024/25 utakaofanyika leo katika boti ya kilimanjaro viii visiwani zanzibar.

Mbali na tukio la jezi Azam watazindua jengo jipya la Michenzani Mall lililopo visiwani humo.

Katika hatua nyingine, kikosi cha Azam FC kinatarajiwa kurejea  leo hii  kutoka Morocco kilipokuwa kimeweka kambi ya wiki tatu kujiandaa na msimu mpya. Azam FC wanatarajiwa kuuanza msimu mpya kwa mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Coastal Union ya Tanga Agosti 8 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Ikiwa Morocco, Azam FC pia ilicheza mechi tatu za kujipima nguvu, Julai 20 ikishinda 3-0 dhidi ya Union Yacoub El Mansour, Julai 27 ikitoa sare ya 1-1 na Union de Touarga, kabla ya kuchapwa 4-1 na Wydad Athletic FC Julai 29.

Azam FC ambayo msimu ujao pamoja na mashindano ya nyumbani pia itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika – itakuwa na safari ya Rwanda pia kucheza na wenyeji,

Chanzo: www.tanzaniaweb.live