Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC kuvaa Jezi Nyeusi Desemba 25

Azam FC Jezi Nyeusi 1140x640 Azam FC kuvaa Jezi Nyeusi Desemba 25

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: Dar24

Afisa Habari wa Azam FC Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ ameibua mjadala mzito katika Mitandao ya Kijamii, kuhusu matarajio ya Kikosi chao kuvaa Jezi Nyeusi wakati mchezo wa Mzunguko wa 18 wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaowakutanisha dhidi ya Young Africans.

Mchezo huo utashuhudia Azam FC wakiwa wenyeji Jumapili (Desemba 25), huku Young Africans wakiwa wametoka kukipiga michezo miwili dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union.

Zaka Zakazi ambaye kwa sasa anatumikia adhabu ya kufungiwa na TFF, amesisitiza kuwa kikosi chao siku hiyo kitavaa jezi nyeusi ili kuwaenzi Wadhamini wao Azam Max.

“Siku ya Krismasi (Kwenye Mechi yao dhidi ya Yanga) tutavaa jezi zetu NYEUSI katika mchezo wetu wa nyumbani dhidi ya Yanga. Tutavaa jezi nyeusi ili kumuenzi Mdhamini wetu AZAM MAX.”

Hata hivyo mjadala huo unaoenakana kuleta mkanganyiko kwa Mashabiki wa Young Africans, ambao wamekuwa na imani za kupata alama tatu kwa uhakika endapo timu yao inavaa Jezi Nyeusi inapocheza Nyumbani ama Ugenini.

Lakini pamoja na mjadala huo kuwa mzito Mitandaoni, Uongozi wa Young Africans haujasema lolote kuhusu ishu hiyo.

Mchezo wa Mzunguko wa Kwanza wa Ligi Kuu uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na kumalizika kwa sare ya 2-2, Azam FC ilivaa Nyeusi huku Young Africans ikivaa Jezi za Kijani.

Chanzo: Dar24