Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC kushusha vyuma vitatu

Azam Simba G.jpeg Azam FC kushusha vyuma vitatu

Thu, 11 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa timu ya Azam FC, umeahidi kusajili wachezaji watatu pekee kwenye dirisha kubwa ili kuimarisha kikosi chao msimu ujao.

Akizungumza nasi, Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema kati ya wachezaji hao watatu tayari wamemalizana na wawili na wanatarajia kuwatambulisha pindi ligi kuu msimu huu utakapo malizika.

“Malengo yetu ilikuwa ni kubeba ubingwa wa mashindano yote ya ndani na kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa asilimia kubwa ya tulichokitarajia hatuja fikia lakini tumeridhishwa na ubora wa wachezaji waliopo ndiomaan benchi la ufundi limeahidi kuongeza wachezaji watatu pekee,” amesema Popat.

Azam FC inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa na pointi 53 lakini pia imetinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na watacheza fainali na mshindi kati ya Singida Big Stars na Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live