Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC kukipiga na Wydad Casablanca ya Mokwena

Azam Mokwena Azam FC kukipiga na Wydad Casablanca ya Mokwena

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam imesema kuwa kwenye kampeni yake ya pre-season, miongoni mwa mechi itakazocheza kujiandaa na msimu ujao ni dhidi ya vigogo wa soka nchini Morocco, Wydad Casablanca, Julai 29, 2024 inayonolewa na kocha Rhulani Mlungisi Mokwena.

Azam ambao wameweka kambi yao nchini Morocco, Jumamosi iliyopita walicheza mechi ya kirafi dhidi ya US Mansour ya nchini humo na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

"Wakati tukiwa kwenye wiki ya mwisho ya maandalizi ya msimu mpya tukiwa kambini nchini Morocco, tunatarajia kucheza mechi mbili za mwisho za kirafiki.

"Tutacheza na Union Touarga, inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika, mchezo utakaofanyika Jumamosi hii saa 2.00 usiku (E.A.T) kabla ya Jumatatu ijayo kucheza na vigogo wa Morocco, Wydad AC kuanzia saa 1.00 usiku (E.A.T)," imesema taarifa ya Azam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live