Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC kujiuliza kwa Ruvu Shooting

Azam Kangwa Kikosi cha Azam kitakuwa uwanjani sambamba na nyota wake waliosamehewa

Thu, 23 Dec 2021 Chanzo: dar24.com

Kikosi cha Azam FC leo Alhamisi (Desemba 23) kinatarajia kuwakaribisha Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi hiyo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Azam FC wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya matokeo ya sare ya 2-2 dhidi ya Mbeya City, yaliyopatikana mwishoni mwa juma lililopiya katika Uwanja wa Azam Complex.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Iddi Abubakar, amesema mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting utakuwa mgumu na wenye upinzani mkubwa kutokana na historia ya timu hizo mbili kila zinapokutana.

“Tumejiandaa vizuri kukabiliana na wapinzani wetu, tumefanyia kazi makosa yetu, na sasa tunaenda uwanjani kupambana na hatimaye kupata kile ambacho tunakitarajia ambacho ni pointi tatu,” amesema Iddi.

Kwa upande wa Ruvu Shooting, Kocha Msaidizi, Mohammed Nakuchema, amesema watakuwa na mabadiliko makubwa ndani ya kikosi chao kwa sababu baadhi ya wachezaji ni wagonjwa na wengine wamekwenda katika kozi.

“Kutokuwepo kwa nyota hao hakutaathiri mipango yetu kwa sababu wachezaji wengine wapo na wako fiti kwa ajili ya kupambana dhidi ya Azam FC, tutazifuata pointi tatu,” amesema Nakuchema.

Nahodha wa Ruvu Shooting, Renatus Ambrose, amesema wanaenda kupambana na ‘kupigana’ ili kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

“Katika mechi iliyopita tumepata matokeo mabaya, kocha ameona makosa yetu na kufanyia kazi kuelekea mchezo wa kesho (leo), tumejiandaa vizuri na tutacheza kwa tahadhari kubwa kutokana na ubora waliokuwa nao wachezaji Azam FC,”amesema Ambrose.

Azam FC inashika nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 12, huku Ruvu Shooting ikiwa nafasi ya 12 ikimiliki alama tisa.

Chanzo: dar24.com