Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC kujipima na Friends Rangers

74386 Azam+pic

Thu, 5 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

AZAM FC  leo usiku watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Friend Rangers ikiwa ni maalumu kwa maandalizi yao kuelekea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Azam na Friend Rangers wanashuka katika dimba la Azam Complex saa moja jioni ambapo kocha msaidizi Idd Cheche amesema mchezo huo ni maalum kwaajili ya kuweka sawa nyota wao kabla ya kuwavaa Triangle United  FC Septemba 13.

Amesema wameamua kucheza mchezo huo mwepesi kwa lengo la kutokuwachosha wachezaji wao na kuweka wazi kuwa wanawaheshimu wapinzani wao na wanategemea mchezo wa ushindani kutoka kwao.

"Mchezo huo ni muhimu sana kwetu tunautumia kuwapima nyota wetu kufahamu ubora wao na mapungufu yao kabla hatujaingia kwenye mchezo wa ushindani na muhimu kwetu kusaka rekodi ya kuvuka hatua inayofuata," amesema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz