Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC kuikaribisha Simba SC Kwa Mkapa

Mkapa Uwanja Azam FC kuikaribisha Simba SC Kwa Mkapa

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: Dar24

Imethibitishwa kuwa Azam FC wamekubali kuhamishia mchezo wao dhidi ya Simba SC Uwanja wa Benjamin Mkapa, badala ya Uwanja wa Azam Complex Chamazi, kama ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara ilivyokua ikionyesha awali.

Azam FC itakua mwenyeji wa mchezo huo namba 72, ambao utapigwa Alhamis (Oktoba 27), huku ukisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Soka nchini Tanzania.

Taarifa ya ratiba ya Michezo ya Mzunguuko ya mzunguuko wa tisa iliyotolewa kwenye Kurasa za Mitandao ya Kijamii ya Bodi ya Ligi ‘TPLB’ imethibitisha mchezo huo kuchezwa Uwanja wa Mkapa, kuanzia saa moja kamili usiku.

Hadi sasa mabadiliko ya Uwanja hayajawekwa hadharani, licha ya Uongozi wa Azam FC kuwahi kusisitiza michezo yao yote ya Ligi Kuu watakayokua nyumbani itachezwa Uwanja wa Azam Complex-Chamazi.

Simba SC inakwenda kukutana na Azam FC ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Mtani wake Young Africans jana Jumapili (Oktoba 23), huku Azam FC ikiambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya KMC FC Ijumaa (Oktoba 21).

Chanzo: Dar24