Azam FC inakumbuka msimu uliopita ilichomolewa kwenye michuano ya CAF ikiwa nyumbani na Al Akhdar ya Libya licha ya kushinda mabao 2-0, kwani awali ililala ugenini 3-0 na leo inashuka tena uwanjani kurudiana na Bahir Dar Kanema ya Ethiopia na kuapa hairudii tena makosa kama hayo.
Wahabeshi hao walioshinda jijini Addis Ababa wikiendi iliyopita kwa mabao 2-1 na wenyeji leo AZAM FC wanahitaji japo ushindi wa 1-0 ili kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kocha Mkuu wa Azam, Youssouph Dabo alisema licha ya wao kupoteza ugenini, bado wana nafasi ya kusonga mbele na tayari amekaa na wachezaji na kuwataka kuwa makini katika kumalizia nafasi wanazozitengeneza kwani ndizo zilizowaangusha Ethiopia.. Kila la kheri Azam