Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC jino kwa jino na Yanga wakiichapa Polisi Tz

Ayoub Lyangaaaaa Azam imepata alama tatu muhimu

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Azam FC imepata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Disemba 5, Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. 

Bao pekee la Azam FC katika mchezo huo limefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 15 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 35 na kurejea nafasi ya pili, ikizidiwa tu wastani wa mabao na mabingwa watetezi, Yanga ambao wana mechi moja mkononi.

Kwa upande wao, Polisi Tanzania ambao leo wameanza kucheza chini ya kocha mpya, Mkongo, Mwinyi Zahera wanabaki na pointi zao tisa za mechi 15 nafasi ya mwisho, 16.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live