Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC hawana wanachoshindania

Yanga Azam F Azam FC hawana wanachoshindania

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi ya Yanga na Azam FC ni miongoni mwa michezo mikubwa kabisa kwenye Ligi ya NBC baada ya Simba vs Yanga, mchezo unaofuata kwa ukubwa na mvuto ni Yanga vs Azam au Simba vs Azam na mechi hizi tatu mara nyingi ndio zimetumika kama kipimo cha ubora wa Ligi yetu.

Ukubwa wa mchezo huu [Yanga vs Azam FC] unaletwa na madaraja ya wachezaji waliopo kwenye timu hizo mbili. Azam FC tangu wamekuja kwenye Ligi wamejaribu kushindana na timu hizi mbili za Kariakoo kwa maana ya kuwa na daraja sawa la wachezaji na benchi la ufundi.

Tofauti ya Azam na timu za Kariakoo ni namna timu hizo zilivyo, Azam FC inakosa kitu cha kushindania! Madaraja ya wachezaji wa Azam hayana tofauti na wachezaji wa timu za Kariakoo lakini ni kwa namna gani wachezaji wanawajibika kutafuta matokeo ndio kitu kinacholeta utofauti.

Yanga na Azam msimu huu zote zimeanza Ligi vizuri, Yanga kupoteza mechi haimaanishi wameanza vibaya kwa sababu timu iliyowafunga msimu huu hata msimu uliopita iliwafunga na bado walichukua ubingwa.

Natarajia kuona mechi ya ushindani kwa sababu mechi imerejea Uwanja wa Benjamin Mkapa, inaweza kuongeza ari na hamasa kwa wachezaji kwa sababu kila mchezaji anatamani kucheza kwenye uwanja mzuri na wenye profile kubwa.

Hizi ni Mechi saba za mwisho walizokutana klabu ya Yanga dhidi ya Matajiri wa Chamazi Azam FC.

Yanga Sc 2 - 0 Azam Fc [ Ngao ya Jamii ]

Yanga Sc 1 - 0 Azam Fc [Fainali ya ASFC]

Azam Fc 2 - 3 Yanga Sc [NBCPL]

Yanga Sc 2-2 Azam Fc [ NBCPL]

Azam Fc 1-2 Yanga Sc [ NBCPL]

Yanga Sc 2-0 Azam Fc [ NBCPL]

Yanga Sc 0-1 Azam Fc [ NBCPL]

Je, Yanga kuendeleza ubabe au Azam kufanya kitu tofauti leo mbele ya wananchi?

Kwa Mkapa patanoga leo!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live