Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC hata wakimchukua Diarra, Aucho, Aziz, bado hawatafika popote

Yanga Azam F Azam FC wafanye haya watafika mbali

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Njia pekee ya kuiangusha Young Africans Sports Club ni kumsajili Eng. Hersi Said na Gharib Said Mohamed (GSM), lakini baada ya miaka kadhaa itanyanyuka tena.

Alikuwepo Yusuf Manji alipoondoka ikatetereka, lakini baada ya ujio wa GSM ikanyanyuka tena mpaka fainali ya CAFCC na unbeaten 49 ndani ya Ligi Kuu.

Njia pekee ya kuifanya Azam iwe timu ya makombe ni kuajiri kiongozi mwenye maono.

Hata umsajili Aziz Ki, Aucho, Diarra na wengine wote, haiwezi kusaidia kitu kwa sababu Azam FC ina Mentality ya timu ndogo. Kuanzia kwa viongozi hadi wachezaji.

Ndiyo maana ni kitu cha kawaida kuona Azam FC wanauma meno dhidi ya Yanga na Simba lakini wanapokutana na timu ndogo ndogo wanapasuka. Maana yake nini?

Mara zote timu ndogo hukamia timu kubwa na hawajitoi kwa kiwango kilekile wanachojitoa wanapocheza na timu kubwa kwa timu ndogo. Hiyo Mentality ya timu ndogo ndiyo inayowatafuna Azam FC.

Solution ni kuondoa hiyo mentality kwa kutafuta viongozi wenye maono, wenye uwezo wa kupandikiza kwa wachezaji na staffs wote wa klabu hali ya kujituma na kuipambania timu kwa jasho na damu katika mechi zote bila kuchagua.

Kutokuwa na mashabiki wengi kwa Azam FC kuwa hali hiyo inafanya wachezaji wakose hamasa kama baadhi ya watu wanavyosema kwangu hiyo sio hoja ya msingi.

Mamelodi Sundowns haina mashabiki wengi lakini imeuangusha utawala wa Kaizer chiefs na Orlando Pirates.

Believe me, hao hao wachezaji waliopo Azam FC kwa sasa wangekuwa Yanga au Simba tayari wangekuwa washainua kwapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live