Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC hao robo fainali Kagame Cup

AZAM FC Kikosi cha Azam FC

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam FC imefanikiwa kutinga hatua ya Nusu fainali ya Mashindano ya kagame Cup baada ya ushindi wa goli 1-0 walioupata siku ya jana dhidi ya Messager Ngozi na Kuongoza Kundi B wakiwa wameshuka dimbani mara mbili na kushinda mara zote na kujikusanyia pointi 6.

Mchezo huo ambao ulipigwa kwenye Dimba la Azam Complex majira ya saa 10:00 jioni ulishuhudia Azam wakiondoka na ushindi huo baada ya goli lililofungwa na Idd Kipwagile 22' kipindi cha Kwanza cha Mchezo.Kwa matokeo hayo Azam Fc tayari wameshatinga hatua ya nusu Fainali hivyo wanasubiri michezo ya kundi A.

Katika Mechi nyingine iliyopigwa siku ya jana katika Uwanja huo huo wa Azam Complex majira ya saa 1:00 usiku kati ya KMKM SC dhidi ya KCCA FC iliisha kwa KCCA FC kuibuka na ushindi wa goli 1-0,goli lililofungwa na Achayi Habert 20'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live