Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC haina haraka na Pyramid, macho yao Ligi kuu

Azam Azammmmmmmmm Mchezaji wa Azam FC, akiwania mpira na wachezaji wa Horseed FC

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Matajiri wa Jiji Azam FC, kupenya katika raudi ya awali kwa kuwatoa timu ya Horseed FC kutoka nchini Somalia, benchi la ufundi la timu hiyo limesema hesabu zao kwa sasa ki kukusanya pointi katika mechi zao zinazokuja mbele kabla ya kushiriki mechi za kombe la Shirikisho Afrika.

Azam ambayo juzi iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Horseed SC ya Somalia hivyo kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa jumla ya mabao 4-1, sasa inasubiri kuwakaribisha matajiri wa Misri, Pyramids katika mechi ya mkondo wa kwanza itakayochezwa Oktoba 15, mwaka huu kabla ya kwenda kurudiana ugenini siku saba baadaye.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati, amesema baada ya kuvuka hatua ya mkondo wa kwanza, akili na nguvu zao sasa ni kwenye mechi tatu za ligi kabla ya kukutana na Pyramids michuano hiyo ya CAF.

Amesema kwa sasa wanaangalia mechi tatu wakianza dhidi ya Coastal Union mchezo utakaochezwa Septemba 27, mwaka huu na baada ya hapo wataenda Kilimanjaro kuwavaa Polisi Tanzania na kisha kurudi Dar es Salaam kumalizina na Yanga.

"Tunahitaji kufanya vizuri msimu huu wa ligi, tupambane kupata pointi zote tisa na baada ya mechi hizo, tutakuwa tumeimarika zaidi na kuanza kufikiri mchezo wetu wa kimataifa dhidi ya Pyramids," amesema Bahati.

Alisema msimu huu malengo yao makubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi katika Ligi Kuu kwa kuvuna pointi muhimu katika kila mechi pamoja na kufanya vizuri michuano ya kimataifa kwa kusonga mbele hadi kucheza hatua ya makundi.

"Mechi za ligi zitatusaidia kuimarika na kuwa bora zaidi kukutana na wapinzani wetu Pyramids, timu yenye uzoefu mkubwa wa michuano hii ya kimataifa na tunahitaji kufanya vizuri kufikia malengo yetu," amesema kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live