Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC haijakata tamaa ya ubingwa Bara

6d902780f7e04774551d59aacb51aabe Azam FC haijakata tamaa ya ubingwa Bara

Thu, 24 Feb 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kocha Msaidizi wa Azam FC, John Matambala amesema timu hiyo bado ina ndoto za kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Matambala alisema hayo juzi baada ya Azam kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United juzi katika Uwanja wa CCM Kirumba mkoani hapa.

Alisema katika raundi ya pili timu yake itapambana ili kushinda michezo yao yote.

“Ligi bado ipo wazi na bado tuna ndoto za kuhakikisha tunachukua ubingwa wa Ligi Kuu. Katika mchezo wetu na Biashara tumetengeneza nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza lakini tulishindwa kuzitumia kabisa,” alisema Matambala.

Alisema walitengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza ila walishindwa kuzitumia, huku wapinzani wao wakitengeneza nafasi mbili tu wakazitumia.

Katika msimamo wa Ligi Kuu, Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza michezo 15.

Timu hiyo imeshinda mechi saba, sare tatu na imepoteza mechi tano.

Azam imefunga mabao 20 na kufungwa mabao 14.

Timu hiyo inarejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Machi Mosi katika Uwanja wa Chamazi. Baada ya mchezo huo, Azam itacheza na Polisi Tanzania katika uwanja huo huo.

Kocha Mkuu wa Biashara United, Vivier Bahati aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam.

Bahati aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi wa Azam kabla ya kutimuliwa hivi karibuni, alisema Azam ubora wao haukuonekana kutokana na ubora waliokuwa nao wachezaji wake.

Chanzo: www.habarileo.co.tz