Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC chali mbele ya Dodoma Jiji

B2F611C0 85D9 4353 A55C 81E116CF825B.jpeg Straika wa Azam Idris Mbombo akigombea mpira na Mchezaji wa Dodoma

Sun, 5 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Dodoma Jiji FC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Muhsin Makame dakika ya 26 na Collins Opare dakika ya 30, wakati la Azam FC limefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 60.

Azam FC ilimaliza pungufu baada ya beki wake Msenegal, Malickou Ndoye kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 42.

Kwa matokeo hayo, Dodoma Jiji wanafikisha pointi 24 na kusogea nafasi ya 10, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 43 nafasi ya tatu baada ya wote kucheza mechi 22.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live