Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC bado weupe tu, walazimishwa sare Chamazi

AZAM FC VS KAGERA Matokeo ya Azam FC hayajawa ya kuridhisa

Sun, 12 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bado jinamizi la mfuendelezo wa matokeo ya ushindi linaendelea kuitafuna Azam FC, baada ya hii leo kulazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar ndani ya dimba la Azam Complex Chamazi.

Mchezo huo wa raundi ya nane Ligi Kuu Bara, ulimshuhudia mshambuliaji hatari wa Azam ambae alikosekana uwanjani kwa kipindi kirefu kutokana na kufanyiwa upasuaji, Prince Dube.

Mpaka dakika 90 zinakamilika, hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na hivyo kugawana pointi.

Matokeo hayo yanatoa ishara mbaya kwa mwalimu George Lwandamina ambae miezi kadhaa aliongezewa Mkataba klabuni hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live