Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC: Tutakwenda kwa adabu zote mbele ya Yanga

Yanga Azam Matokeo Azam FC: Tutakwenda kwa adabu zote mbele ya Yanga

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa wataingia uwanjani kwa tahadhari kubwa wakiwaheshimu wapinzani wao, Yanga SC kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la NBC, mchezo unaotarajiwa kupigwa Jumapili, Juni 2, 2024 katika Dimba la Amaan Zanzibar.

Msimu huu Yanga na Azam wamekutana mara tatu huku Yanga akishinda michezo miwili (mmoja ngao ya jamii 2-0 na mmoja wa ligi 3-2) na Azam akishinda mchezo mmoja wa Ligi 2-1.

“Tunaliendea Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘CRDBFC’ kwenye Fainali kwa heshima adabu sana, kwa sababu tunajua aina ya timu ambayo tunakutana nayo huko, kwa hakika hautakuwa mchezo rahisi lakini tumejipanga kupambana na kufikia lengo tuliojiwekea.

“Sisi tunachoamini sio kuhusu wao walivyo bali ubora wetu, hivyo tutaenda na adabu mno mbele yao kwa sababu tuna maandalizi mazuri na tumecheza vizuri karibuni na hatujakaa muda mrefu bila kucheza tunaamini ni sababu tosha ya kufikia lengo na kutwaa taji hilo,” amesema Hasheem Ibwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live