Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC: Tunakuja na kikosi kazi kazi

Azam FC VS MAPINDUZI Azam FC: Tunakuja na kikosi kazi kazi

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Azam FC umeweka wazi kuwa msimu ujao wanakuja na kikosi kazi kazi kitakachokuwa na maboresho kwenye idara nyingi.

Tayari Azam FC imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Feisal Salum aliyekuwa anacheza Young Africans.

Afisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe, amesema kuwa, waliokuwa wanawabeza sasa wanaona ukweli ulivyo na wanaendelea na maboresho.

“Wapo waliokuwa wanatubeza kuhusu mipango yetu na ilipokamilika wamekaa kimya, sasa tunakwenda kufanya maboresho mengine.

“Ukweli ni kwamba kila kitu ni mipango na Azam FC ni timu kubwa lazima tufanye mipango kwa umakini kupata tunachostahili mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema lbwe.

Chanzo: Dar24