Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam Complex katika ramani ya Viwanja vya Soka Afrika

AZAM AZAMMMM sehemu ya Uwanja wa Azam Complex

Fri, 17 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uwanja wa Klabu ya Azam FC, Azam Complex umekaa kwenye ramani ya viwanja vya soka barani Afrika baada ya vilabu kadhaa kuomba kufanyia mazoezi katika uwanja huo na baadhi kuomba kuutumia katika mechi zao za nyumbani kama wenyeji japokua si timu kutoka ndani ya Tanzania.

Awali baadhi ya Timu zilipendekeza kuutumia uwanja wa Uhuru kwa mechi zao kama wenyeji lakini mpaka hivi sasa wameshapeleka maombi na kubadilishiwa kuutumia uwanja wa Azam Complex na sababu kubwa imetajwa kuwa ni ubora wa miundombinu ya uwanja huo.

Klabu ya Biashara United kutoka Tanzania ambao wanashiriki Kombe la Shirikisho Afrika imefanya mazoezi katika uwanja huo siku ya jumatano ikijiandaa na mechi yake ya marudiano dhidi ya Dikhil FC kutoka Djibouti, hali kadhalika pia klabu hiyo ya Djibout imefanya mazoezi yake katika uwanja wa Azam Complex.

Klabu nyingine zilizoutumia uwanja huo kwa maandalizi ya mechi zao za kimataifa ni pamoja na Azam FC wenyewe kutoka Tanzania, Horseed SC (Somalia), Le Messager de Ngozi (Burundi), US Gendermarie (Niger).

Zaidi ya kufanya mazoezi, timu hizi pia zitautumia uwanja huu kwa mechi zao, ambapo;

Septemba 17, Saa 10 alasiri, Le Messager de Ngozi watacheza dhidi ya US Gendermarie.

Huu ni mchezo wa mkondo wa pili raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa, Mchezo wa kwanza uliisha 1-1.

Timu za Burundi zinautumia uwanja wa Azam Complex kama uwanja wao wa nyumbani kwa sababu CAF imezuia mechi kufanyika Burundi kutokana na hali ya maambukizi ya Uviko 19.

Septemba 18, Saa 10 alasiri, Horseed SC dhidi ya Azam FC mechi ya mkondo wa Pili Kombe la Shirikisho Afrika, na majira ya saa moja usiku, Biashara United Mara dhidi ya Dikhil FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live