Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam, APR zapishana

Popat Azam Nsz Azam, APR zapishana

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam FC inatarajia kuelekea Rwanda kucheza mchezo wa kirafiki Agosti 3, mwaka huu, dhidi ya wenyeji wao, Rayon Sports, hivyo itapishana na wapinzani wao kwenye mechi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, APR ambao siku hiyo watakuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kumenyana na Simba.

Ikumbukwe, Rayon Sports ndio mpinzani mkubwa wa APR kwenye Ligi Kuu ya Rwanda huku pia Simba wakiwa wapinzani wa Azam kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Azam watacheza na Rayon Sports kwenye tamasha la timu hiyo ili kujaribu kupata ladha ya soka la Rwanda kabla ya kuvaana na APR mwezi ujao.

Wakati Azam wakiwa huko, APR itamenyana na Simba kwenye tamasha lao la kila mwaka la Simba Day, ambalo klabu hiyo ya Tanzania hulitumia kutambulisha kikosi na benchi lao la ufundi kuelekea msimu mpya.

Akizungumza na Nipashe jana, msemaji wa Azam FC, Hasheem Ibwe, alisema timu hiyo itaondoka Morocco baada ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Wydad Casablanca jana.

"Baada ya mchezo huo tutaondoka moja kwa moja kuelekea Rwanda, mchezo huu dhidi ya Rayon Sports ni muhimu sana kwetu, tunaenda kupata ladha ya soka la Rwanda kuelekea mchezo dhidi ya APR," alisema Ibwe.

Alisema baada ya mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports, Azam itarejea nchini kwa ajili ya mchezo wao wa Ngao ya Jamii hatua ya nusu fainali dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Agosti 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: