Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ayoub hawezi kumweka benchi Manula - Jemedari Said

Manula Ayoub Ayoub hawezi kumweka benchi Manula - Jemedari Said

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini kupitia EFM, Jemedari Said Bin Kazumari amesema kipa wa Klabu ya Simba, Ayoub Lakred hana uwezo wa kumuweka benchi Aishi Manula iwapo atapona majeraha yake.

Kauli hiyo ya Jemedari inakuja baada ya Simba kutoa sare ya bao 2-2 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia juzi Jumamosi, Septemba 16, 2023 wakati wa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa katika Dimba la Levy Mwanawasa nchini humo huku Lakred akifanya kosa lililozaa bao la 2.

“Tukikaa wenyewe hapa tuambiane, akipona Aishi Manula akawa yuko sawa sawa, ukiwaweka wawili na Ayoub nani ambaye utampa nafasi? Kisha utajiuliza kwamba, je, kulikuwa na sababu ya kumsajili?

“Sijasema ni kipa mbaya, Ayoub wanasema ni bora sio akiwa Simba ni akiwa huko alikotoka,” amesema Jemedari Said.

Baada ya Manula kuumia, Simba sasa ina makipa wanne (Ayoub Lakred wa Morocco, Ally Salim, Ahmed Feruzi, Hussein Abel) pamoja na Manula mwenyewe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: