Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ayoub ameibeba mechi - Ahmed Ally

Ahmed Ally: Twendeni Uwanjani Hata Kama Tuna Hasira.jpeg Ayoub ameibeba mechi - Ahmed Ally

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Semaji la CAF, Ahmed Ally amesema, Ayoub Lakread ni miongoni mwa wachezaji wa Simba SC ambao wameibeba timu dhidi ya Wydad Casablanca kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar leo Desemba 19, 2023

Mbali na Ayoub, Ahmed amesema Willy Onana, amethibitisha kile alichowahi kukisema kuwa ni mcheza mkubwa na mchezaji wa zamani Samwel Etoo ndiye aliyewashauri Simba kumchukua.

"Ayoub amefanya maajabu, Onana imechukua takriban miezi mitano kuthibitisha kile nilichowahi kuwaambia Watanzania kwamba Etoo mwenyewe alitushauri tumsajili," alisema Ahmed.

Kwenye mechi ya leo ambayo Simba iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Wydad Casablanca, Ayoub alifanya save za hatari ambapo kama si mahiri wake, tungekuwa tunazungumza mengine usiku huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live