Wed, 24 Jul 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Kipa namba moja wa Simba SC, Ayoub Lakred anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki sita baada ya kuumia katika kambi ya timu hiyo nchini Misri.
Ayoub ambaye ameongezewa mkataba na Simba hivi karibuni, amepata majeraha ya nyama za Paja zitakazomuweka nje kwa kipindi hicho.
Kitendo cha Ayoub kuumia kunafanya Simba SC ibakiwe na makipa wawili ndani ya kambi hiyo ambao ni Ally Salim na Hussein Abel.
Uongozi wa Simba uko mbioni kumuwahisha nchini humo golikipa, Aishi Manula ambaye hakuwa sehemu ya kambi.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live