Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ayoub Lakred arejea Simba

Lakred Ayoub Trsns Ayoub Lakred

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Simba, Ayoub Lakred amerejea na kuanza mazoezi leo Uwanja wa MO Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya watani, Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini.

Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kwamba Lekred alikwenda kwao, Morocco baada ya mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Al Ahly Jijini Cairo nchini Misri Aprili 5, mwaka huu kwa sababu ya matatizo ya kifamilia.

Aidha, Ahmed Ally amesema kikosi kitaondoka mapema leo kwenda visiwani Zanzibar kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live