Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Awesu amnyoshea mikono Pacome

Pacome Z Aweso Awesu amnyoshea mikono Pacome

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo kutoka visiwani Zanzibar Awesu Awesu amesenma anavutiwa na kiwango cha Kiungo Mshambuliaji wa Young Africans, Pacome Zouzoua na amekuwa akimfuatilia kila timu yake inapocheza.

Awesu anayeitumikia KMC FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara amesema kuna vitu vingi amekuwa akijifunza kutoka kwa raia huyo wa lvory Coast ikiwemo namna ya kuichezesha timu na kufunga mabao.

“Ukweli kwa wachezaji wa kigeni hasa katika eneo la kiungo navutiwa sana na kiungo wa Young Africans, Pacome, jamaa anajua sana mpira nimekuwa namfuatilia kwa karibu na kuna vitu vingi naiga kutoka kwake,” amesema Awesu.

Kiungo huyo aliyecheza timu nyingi kwenye Ligi ya Tanzania Bara, amesema wapo wengine wanaomvutia akiwemo Maxi Nzengeli na Fabrice Ngoma wa Simba SC, lakini Pacome ndio mtu anayemvutia kwa kiasi kikubwa.

Kiungo huyo alijiunga na Young Africans msimu huu akitokea Asec Mimosas na tayari amefunga mabao saba katika michuano yote ambayo Young Africans inashiriki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live