Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Avunja mkataba na Zamalek kisa msongo wa mawazo

Zakaria El Wardi 1661246460.jpeg Zakaria Al-Wardi

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Zamalek ya Misri imetangaza kusitisha mkataba wa mchezaji Zakaria Al-Wardi, baada ya mchezaji huyo kuwaambia viongozi wa klabu hiyo kuwa anasumbuliwa na msongo wa mawazo, hali inayomfanya ashindwe kusalia klabuni hapo.

Kiungo huyo wa zamani wa Raja Casablanca mwenye umri wa miaka 24 alijiunga na Zamalek mwezi Agosti mwaka huu

"Tunamshukuru Zakaria Al-Wardi kwa muda aliokaa nasi, atarudisha pesa alizochukua na kukatisha mkataba kwa makubaliano" sehemu ya taarifa ya Zamalek.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live