Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aveva ashindwa kufika mahakamani, akwamisha hukumu yao

Aveva Pic Data Aliyekuwa Rais wa Klabu ya soka ya Simba, Evans Aveva

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Hukumu ya kesi ya aliyekuwa Rais wa Klabu ya soka ya Simba, Evans Aveva na aliyekuwa makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’ imekwama baada ya Aveva kushindwa kufika mahakamani.

Hukumu hiyo ilikuwa imepangwa kutolewa leo Jumatano, Oktoba 6,2021 na Hakimu Mkazi Mkuu Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dar es Salaam , Kisutu, Thomas Simba.

Hata hivyo kutokana na Aveva kutokuwepo mahakamani, mahakama hiyo imeshindwa kusoma hukumu hiyo na badala yake imeiahirsha hadi Oktoba 21, mwaka huu.

Kaburu ambaye ndiye pekee aliyefika mahakamani kusikiliza hukumu hiyo ameieleza mahakama hiyo kuwa Aveva ameshindwa kufika mahakamani kwa kuwa yuko hospitalini, Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) kwa ajili ya kliniki.

Kaburu amesema kuwa Aveva anahudhuria kliniki hiyo kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.

Hakimu Simba amekubaliana na maelezo hayo ya Kaburu na akaiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 21, mwaka huu, saa 3:00 Asubuhi kwa ajili ya kusomwa hukumu hiyo.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na kesi ya jinai yenye jumla ya mashtaka manane yakiwemo ya kughush nyaraka, matumizi mabaya ya madaraka na kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya Benki ya klabu hiyo bila idhini ya Kamati ya Utendaji ya Simba.

Vigogo hao wa zamani wa  Simba wanadaiwa kuhamisha fedha hivyo zilizotokana na mauzo ya aliyekuwa mchezaji wake Emmanuel Okwi aliyeuzwa kwa Klabu ya Etoile Sportive Du Sahel ya nchini Tunisia.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz