Thu, 28 Oct 2021
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu kifungo cha nje cha miezi sita aliyekuwa Rais wa Simba, Evans Aveva kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi.
Wakati Aveva akihukumiwa kifungo hicho, aliekuwa makamu wake, Godfrey Nyange maarufu "Kaburu" akiachiwa huru baada ya mahakama hiyo kutomkuta na hatia.
Viongozi hao wa juu wa zamani wa Simba wamehukumiwa baada ya hukumu hiyo kuahirishwa mara kadhaa.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live