Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aussems kicheko tu

43554 Pic+aussems Aussems kicheko tu

Mon, 25 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa Simba SC, Mbelgiji Patrick Aussems amewasifu vijana wake kwa viwango walivyovionyesha katika michezo migumu mfululizo waliyocheza hivi karibuni kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Aussems alisema ushirikiano wake mzuri na wachezaji wake ni miongoni mwa vitu ambavyo vimechangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kuendelea kuimarika kadri siku zinavyosogea.

“Tunaweza kuendelea kufanya makubwa, kinachoweza kuendelea kutusaidia ni ushirikiano baina yetu, kunapokuwa na michezo mingi mbele tena migumu kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko ya kikosi.

“Mabadiliko hayo husaidia kupumzisha wachezaji kutokana na idadi ya mechi zilizopo mbele, nilifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya African Lyon, nimeona uwajibikaji kwa mchezaji mmoja mmoja ukiongezeka, hilo limenivutia,” alisema kocha huyo.

Michezo hiyo migumu na mfulizo ambayo Aussems alikuwa akiizungumzia ni dhidi ya Al Ahly ambao walishinda kwa bao 1-0, Februari 12 na mara baada ya kumalizana na waarabu hao, Februari 16 wakakabiliana na watani wao wa jadi, Yanga ambao na wenye waliwalaza kwa bao 1-0.

Baada ya michezo hiyo miwili mfululizo wakacheza na African Lyon jijini Arusha kabla ya kukumbana na Azam juzi uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam ambapo waliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1.

Simba inatarajiwa kucheza tena mchezo wake mwingine wa kiporo cha Ligi Kuu Tanzania Bara, Jumanne ya Februari 26 dhidi ya Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Samora.



Chanzo: mwananchi.co.tz