Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aussems atuliza mzuka Msimbazi

95059 AUSEMS+PIC Aussems atuliza mzuka Msimbazi

Mon, 10 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

UPEPO haupo sawa Simba, kwani Kocha Mkuu wao, Sven Vandenbroeck hatma yake ipo mashakani kutokana na matokeo na hata soka la timu yake wakati pia mashabiki wa wekundu hao wakimkumbuka kocha aliyemtangulia Patrick Aussems, ambaye amewatuliza mashabiki kwa kuwapa ujumbe murua.

Akizungumza na Mwanaspoti katika mahojiano maalumu akiwa Ufaransa, Aussems alisema anafuatilia sana maendeleo ya timu yake kila mchezo akiwa kwake na anajua kila kinachoendelea.

Kocha huyo alisema katika kila mchezo unapomalizika amekuwa akipokea tathmini mbalimbali za mashabiki wa timu yake wakimkunbuka na kumtaka kurejea.

“Simba ipo katika moyo wangu kuna kazi nzuri nilifanya pale kwa hiyo naifuatilia sana kila inapocheza.

Kuna wakati nilipoondoka tu wakati inashinda wapo ambao walikuwa wananitumia maneno makali lakini sikuwa na tatizo nao,” alisema Aussems.

Alisema kwa sasa amekuwa akipokea ujumbe mbalimbali mwingi katika simu yake kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo wakimtaka kurejea haraka kazini lakini amekuwa akikosa cha kuwajibu.

Pia Soma

Advertisement
Raia huyo wa Ubelgiji alisema ujumbe mbalimbali pekee anaoweza kuwapa mashabiki wa timu yake ni kwamba anawahurumia na wakati mgumu wanaokutana nao sasa na hata mwenyewe mwenendo huo unamkosesha raha.

“Naona sasa mambo hayaendi vizuri kwa sasa, nimekuwa nikipokea ujumbe mwingi wa mashabiki wakiniomba kurejea Simba kila mechi za karibuni zinapomalizika. Kama mtu ambaye nilishi nao kwa amani inaniumiza pia sio rahisi kufurahi unapoona sehemu ambayo ulifanya kazi vizuri mambo hayaendi vizuri inaumiza sana.”

Aidha Kocha huyo alisema baada ya mchezo wa juzi kati ya Simba na JKT ambapo WEkundu hao walilala baop 1-0, anajua kwamba Mwenyekiti wa Bodi ya klabu hiyo, Mohammed Dewji ‘MO’ anaumia zaidi na hali hiyo lakini amemtaka kutulia na kutanguliza subira katika wakati huu.

“Kuna wakati nilishtuka niliposikia ameamua kujiondoa kama Mwenyekiti wa Bodi, haikuwa taarifa nzuri kabisa kwa simba lakini baadaye naona alibadili uamuzi wake.

Kwa sasa najua hali ya timu itakuwa inamsumbua kama mtu ambaye anaweka nguvu kubwa ni kama shabiki au kiongozi yeyote lakini nimemtumia ujumbe naona anahitaji kutulia zaidi asikate tamaa,” alifichua Aussems.

Chanzo: mwananchi.co.tz