Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aussems, Bocco wateka tuzo Ligi Kuu Bara

56346 Pic+tuzo

Wed, 8 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems na straika wake, John Bocco wamechaguliwa kuwa washindi wa Tuzo za Ligi Kuu Bara kwa mwezi Aprili hii ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwa Aussems na Bocco ambao walichukua pia mwezi uliopita wa Machi. Washindi haoo wanabeba kikombe pamoja na pesa kiasi cha Sh. 1 milioni na kisumbusi cha Azam TV.

Tuzo hizo hizo zimekuwa zikitolewa kila mwezi ambapo kwa sasa  wadhamini ni Biko Sports ambao ndio wanatoa kiasi hicho cha pesa na Azam ambao wana haki ya matangazo.

Washindi wengine wa tuzo hizo kwa miezi iliyopita katika msimu huu upande wa wachezaji ni  Mnyarwanda Meddie Kagere (Agosti, Februari), mshambuliaji wa Mbeya City Eliud Ambokile (Septemba), mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi (Oktoba), Makambo (Novemba, Desemba) Dickson Ambundo wa Alliance FC (Januari) na Bocco (Machi na Aprili)

Kwa upande wa makocha walioshinda tuzo hiyo kwa msimu huu ni Amri Said alipokuwa na Mbao FC (Agosti), Mwinyi Zahera wa Yanga (Septemba), Hans Pluijm wa Azam FC (Oktoba) na Mwinyi Zahera (Novemba).  Kocha wa KMC, Etiene Ndayiragije (Januari)   Kocha wa Prisons ya Mbeya, Mohammed Rishard (Februari), Patrick Aussems (Machi na Aprili)

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz