Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho yamkuta mengine Uganda

Khalid Aucho?fit=760%2C558&ssl=1 Aucho yamkuta mengine Uganda

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Uganda itakabiliana na Somalia katika mchezo wake unaofuata wa kundi G la kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia ambao utachezwa katika Uwanja wa Manispaa ya Berkane, Morocco.

Uganda imeanza vibaya harakati za kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza kwenye kundi G dhidi ya Guinea kwa mabao 2-1.

Ikiongozwa na nahodha Khalid Aucho anayeitumikia Yanga, Uganda ilijikuta ikiruhusu bao la dakika za majeruhi la Seydouba Cisse katika dakika za nyongeza za kipindi cha pili, lililowahakikishia wenyeji mwanzo mzuri kwenye kundi lao.

Bao hilo la ushindi la Guinea lilikuwa la kwanza kwa Cisse anayeitumikia Leganes ya Hispania na alifunga baada ya kuingia uwanjani akitokea benchi katika dakika ya 80 akichukua nafasi ya Abdoulaye Toure katika mchezo huo, Guinea walitangulia kupata bao la kwanza mapema dakika ya 10 kupitia kwa Aguibou Camara lakini Uganda walisawazisha katika dakika ya 30 kupitia kwa Bayo Fahad.

Kichapo hicho cha ugenini kutoka kwa Guinea kimeifanya Uganda iwe nafasi ya tano katika msimamo wa kundi G lenye timu sita likiongozwa na Algeria ambayo jana iliichapa Somalia kwa mabao 3-1.

Kwa Aucho, kichapo hicho kimemkuta katika siku ambayo kamati ya usimamizi na uendeshaji ya Bodi ya Ligi Kuu imempa adhabu ya kumfungia michezo mitatu na faini ya Shilingi 500,000 kwa kosa la kumpiga kiwiko Ibrahim Ajibu katika mchezo baina ya Coastal Union dhidi ya Yanga, Novemba 8.

Chanzo: Mwanaspoti