Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho rasmi Yanga

Aucho Pic Data Mchezaji anaetajwa kusainiwa na Yanga, Khalid Aucho (Kulia) akiwasili Jijin Dar es Salaam

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) ni kama wanafanya komesha, kwani kile wanachokifanya kwa sasa ni balaa na wapinzani wao lazima washtuke, ikiwa hata saa 24 hazijatimia tangu imshushe kipa kutoka nchini Mali, Diarra Djigui waliyemtambulisha rasmi jana, wamemleta nyota mwingine mpya Khalid Aucho kininja na kumaliza ubishi uliokuwapo awali juu yake kama atatua Jangwani au Msimbazi.

Mabosi wa Jangwani mwishowe wakaipiga bao Simba kwa kumshusha kiungo huyo mkabaji kutoka Uganda kwa Wananchi hao wa Jangwani ni kama wana kitu wanatengeneza kuelekea msimu ujao, kwa staili yao ya sasa kushusha nyota kadhaa, kwani jana ilishusha staa wao wa nne wa kigeni lakini huyu wakimshusha kininja wakiwahofia Simba, iliyokuwa ikitajwa nayo kumvizia.

Katika mitandao yao ya kijamii,Timu ya Yanga imeweka jumbe zinazoonesha ama kuwataka Mashabiki wake na wapenda soka kuwa karibu na waweke bando wasije kusema hawakuambiwa.

Chanzo: Mwanaspoti