Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho ndani, Gamondi akiwaacha watatu Dar

Bakari X Okrah X Bacca Aucho ndani, Gamondi akiwaacha watatu Dar

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga imesafiri ikienda Bukoba kuifuata Kagera Sugar, lakini msafara wake umewaacha nyuma mastaa watatu, huku Khalid Aucho akirejea kikosini.

Awali, Aucho alikumbana na rungu la Bodi ya Ligi baada ya kubainika kumpiga kiwiko beki mmoja wa Coastal Union wakati timu hizo zilipokutana kwenye Uwanja wa Mkwakwani - Tanga, na Yanga kushinda kwa bao 1-0.

Kikosi cha Yanga kilichoondoka alfajiri leo kikipitia Mwanza kabla ya kuunganisha kwenda Bukoba kimeondoka na msafara wa wachezaji 20.

Katika msafara huo timu hiyo imewaacha mabeki wawili wa kati, nahodha Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Hamad 'Bacca'.

Yanga imelazimika kuwaacha mabeki hao baada ya kupimwa na kugundulika kuwa na majeraha madogo, wakibakizwa Dar ili wapone vizuri.

Kocha Miguel Gamondi amesema mabeki hao wataendelea na matibabu akiamini kikosi alichoondoka nacho kitaweza kupigania pointi tatu.

Mbali na mabeki hao Yanga pia imemuacha kiungo mpya mshambuliaji Augustine Okrah ambaye hajafanikiwa kuwa sawa baada ya kutoka kwenye majeraha.

"Tungeweza kwenda nao, lakini ni vyema wakapona sawasawa. Wachezaji tunaoondoka nao tunaamini wataweza kupigania ushindi wa timu," amesema Gamondi.

Yanga itakucheza na Kagera Sugar kesho saa 10 jioni kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Wachezaji 20 walioondoka ni pamoja na makipa Aboutwalib Mshery na Metacha Mnata; mabeki ni Yao Attohoula, Joyce Lomalisa, Dickson Job, Gift Fred, Nickson Kibabage na Kibwana Shomari.

Kwa upande wa viungo kuna Zawadi Mauya, Pacome Zouzoua, Jonas Mkude, Maxi Nzengeli, Farid Mussa, Aucho, Salum Abubakar 'Sure boy', Mahalatse Makudubela 'Skudu', Shekhan Khamis huku washambuliaji wakiwa ni Joseph Guede, Kennedy Musonda na Clement Mzinze.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 30, huku Kagera Sugar ikiwa nazo 13 ikishika nafasi ya 14.

Chanzo: Mwanaspoti