Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho na Mayele Kuwakosa Taifa Jang’ombe Leo

YANGA MAYELE MOLOKO FEI TOTO Aucho na Mayele Kuwakosa Taifa Jang’ombe Leo

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MASTAA wa Yanga, Khalidi Aucho na Fiston Mayele, hawatakuwa sehemu ya mchezo wa leo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Taifa Jang’ombe na kwamba wataunguruma dhidi ya KMKM kesho kutwa Ijumaa.

Aucho ameshindwa kusafiri na kikosi hicho kufuatia kuomba ruhusa ya kwenda kwao Uganda kwa ajili ya kuiona familia yake, huku Fiston Mayele naye yupo nchini DR Congo, kwa ajili ya kuhani msiba wa shemeji yake na anatarajiwa kuungana na timu mapema Alhamisi.

Aucho na Mayele wameshindwa kuambatana na timu iliyoondoka jana jioni kwa kuwa wote wamesafiri kwenda makwao hivyo wanatarajia kuungana na kikosi mapema Alhamisi ya Januari 6, mwaka huu.

“Aucho sio sehemu ya msafara pamoja na Mayele kwa kuwa wote wapo makwao, hivyo tunatarajia watakuwa nasi katika mchezo dhidi ya KMKM unaotarajiwa kupigwa Januari 7, mwaka huu, hivyo nina imani kutokana na ratiba zao zilivyo watawahi na huenda wakawa sehemu ya mchezo wetu siku hiyo,” kilisema chanzo hicho.

Yanga wanakwenda kushiriki michuano hiyo wakiwa mabingwa watetezi wakiifunga Simba kwenye fainali ya mwaka jana kwa penalti 4-3 baada ya kutoka suluhu.

Yanga wenyewe tayari wametambulisha wachezaji wapya watatu ambao ni Salum Aboubakari ‘Sure Boy’ kutoka Azam FC, Denis Nkane (Biashara United) na Abdoultwalib Mshery (Mtibwa Sugar).

Bwalya aliyewahi kuichezea Al Ahly ya nchini Misri, hivi karibuni alitangaza kuvunja mkataba na timu ya Yeni Malatyaspor baada ya kutolipwa mshahara kwa miezi minne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live