Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho kujazwa minoti

Khalid Aucho?fit=760%2C558&ssl=1 Aucho kujazwa minoti

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi za mwisho kundi F kufuzu Afcon 2024 zitapigwa kesho saa 4:00 usiku katika viwanja viwili tofauti ambapo Tanzania (Taifa Stars) ikiwa ugenini Algeria itasaka ushindi au sare kujihakikishia nafasi ya kufuzu huku Niger ikiikaribisha Uganda.

Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) limeboresha maslahi ya wachezaji wake ambao awali posho ya siku ilikuwa Sh1.2 milioni ya Tanzania (Sh1.8 milioni ya Uganda) na sasa imeongezeka kufikia Sh1.8 milioni ya Tanzania.

Kubwa zaidi ni endapo watashinda mechi ya Niger na kufanikiwa kufuzu kila mchezaji na benchi la ufundi atabeba Sh12 milioni ya Tanzania.

Tanzania ina pointi saba katika kundi hilo ambapo ushindi au sare itafuzu huku Uganda ikijitaji ushindi wa mabao mengi huku ikiiombea Taifa Stars dua mbaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: