Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho awaonya wanaomchezea rafu za makusudi

Aucho Topee Aucho awaonya wanaomchezea rafu za makusudi

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mkabaji wa Klabu ya Yanga, Khalid Aucho 'Daktari wa Mpira' amesema kuwa iwapo watu wanataka awe mtu mbaya basi atafanya hivyo.

Aucho ambaye ametoka majeruhi aliyokaa kwa mwezi mzima ametoa kauli hiyo ikiwa ni mechi tatu mfululizo akifanyiwa, mmadhambi (fouls) za makusudi huku akiamini kuwa kisasi ni haki.

Mechi ya juzi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la NBC dhidi ya Tabora, Aucho alishindwa kuendelea.

Jana Aucho aliandika maneno haya akimnukuu Zlatan Ibrahimovic; “Ikiwa unataka niwe mtu mzuri nitakuwa mtu mzuri na ikiwa unataka niwe mtu mbaya pia nitakuwa mtu mbaya,” amesema Aucho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live