Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho awagawa wadau tuzo za TFF

Khalid Auchoooooooo Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kitendo cha jina la kiungo wa Yanga, Khalid Aucho kutokuwa kwenye orodha ya wachezaji walioteuliwa katika kikosi bora cha msimu uliopita wa 2023/24 kimewaibua wadau mbalimbali wa soka la Tanzania na kutoa maoni tofauti huku wengi wakiamini Mganda huyo alistahili.

Pazia la Ligi Kuu Bara msimu uliopita lilifungwa rasmi juzi, Jumatatu ya Agosti Mosi jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Super Dome Masaki ambako zilifanyika sherehe za tuzo za msimu huo.

Ishu ya Aucho, imeonakana kuzua mjadala pamoja na muonekano wa baadhi ya tuzo kama vile ile ya mfungaji bora na hata kipa bora kutokuwa na utofauti wowote kama ilivyokuwa kwa mataifa yaliyoendelea huku ikilinganishwa na thamani ya ligi kwa sasa.

Licha ya kuheshimu mchango wa Mudathir Yahya na maamuzi ya kamati ya tuzo, nyota wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua anaamini kuwa Aucho alistahili kuwa kwenye kikosi bora cha msimu.

Chambua alisema Mganda huyo ndiye namba sita wake bora msimu uliopita na ni wazi kuwa aliipa Yanga uhai katika eneo la kiungo tofauti na Mudathir ambaye alitumika zaidi katika kushambulia.

"Mudathir ni mchezaji mzuri sana lakini msimu uliopita hakutumika kama kiungo mkabaji, nadhani Aucho ndiye alistahili kuwa katika kikosi bora cha msimu kwa kigezo hicho kulingana na nafasi kama ilivyokuwa kwa wachezaji wengine ambao wamechaguliwa," alisema na kuongeza;

"Nadhani Mudathir alitakiwa kushindanishwa na wachezaji wa namba nyingine na hakupaswa kutazamwa kama namba sita lakini lazima tujue wanakamati nao ni binadamu na wanavigezo vyao katika machaguzi yao, wamefanya kazi kubwa mapungufu ni mchache."

Kwa upande wake, nyota wa zamani wa Simba, Zamoyoni Mogella hakutaka kuwa upande wowote zaidi aliheshimu maamuzi ya kamati kwa kusema wamefanya uchaguzi kwa vigezo vyao hivyo sio sawa kukosoa wakati hajui vigezo hivyo ni vipi.

"Nipo katikati naweza kusema Aucho alistahili au hakustahili, kwa sababu undani wa machaguo ya kikosi bora wanajua wanakamati," alisema kwa kifupi.

Naye kocha wa timu za vijana wa Azam FC, Mohammed Badru alisema mbali na Aucho alihoji pia tuzo ya kiungo bora, anaamini kuwa Feisal Salum alistahili na wala hakuna na shida juu ya uteuzi wa Stephane Aziz Ki kuwa mchezaji bora wa msimu 'MVP'.

"Kila mtu amekuwa akisema lake, kwanza tupongeze kamati kwa kazi kubwa waliyofanya, mapungufu ni machache sana naamini tuzo za msimu ujao zitakuwa bora zaidi, kwangu Aucho alitakiwa kuwa sehemu ya kikosi bora cha msimu na hata Fei nadhani ndiye kiungo bora," alisema.

Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' alisema wachezaji wa Tanzania wanatakiwa kujituma wimbo anaouimba kila siku na ndio maana wageni wengi wanatwa tuzo.

"Ubora na uwezo aliokuwa nao Ibrahim Ajibu hata Chama anasubiri sema kwa kuwa mwenzake anajua nini anafanya na ndio maana kila siku amekuwa akiongelewa," alisema.

WASHINDI WA TUZO 2023/24

Mshindi tuzo ya mfungaji bora Kombe La Shirikisho la CRDB imekwenda kwa Clement Mzize -Yanga

Mshindi tuzo ya Kipa Bora Kombe La Shirikisho la CRDB, Djigui Diarra – Yanga

Mshindi tuzo ya mchezaji Bora Kombe La Shirikisho la CRDB, Feisal Salum – Azam FC

Mfungaji Bora Ligi Kuu Bara 2023/2024

Stephan Aziz Ki- Yanga

Mshindi tuzo ya Kocha Bora Ligi Kuu Bara 2023/24

Miguel Gamondi – Yanga.

Mchezaji Bora Ligi Kuu Bara 2023/24

Aziz KI – Yanga.

Mshindi wa tuzo ya Beki bora Ligi Kuu Bara 2023/24

Ibrahim Bacca (Yanga).

Mshindi kipa bora wa mwaka, Ley Matampi (Coastal Union).

Kiungo Bora wa mwaka Aziz KI (Yanga).

Mchezaji bora chipukizi Ligi Kuu Bara, Shomary Raheem (KMC).

Mwamuzi Msaidizi Bora Ligi Kuu 2023/24

Mohammed Mkono.

Mwamuzi Bora Ligi Kuu 2023/24

Ahmed Arajiga.

Timu yenye nidhamu (Mtibwa Sugar).

Tuzo ya kamishna bora, Hamis Kitila (Singida).

Mchezaji Bora wa Tanzania anayecheza nje (Me)

Mbwana Samatta.

Mchezaji Bora wa Tanzania anayecheza nje (Ke), Aisha Masaka.

Chanzo: Mwanaspoti