Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho awaahidi Yanga burudani, Soka safi

KHalid Aucho Fundii Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho

Thu, 14 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mkabaji mpya wa Yanga, Mganda, Khalid Aucho,amewaambia mashabiki kuwa watarajie kuona soka safi la pasi linalochezwa katika baadhi ya klabu kubwa Ulaya kwenye michezo ijayo wa Ligi Kuu Bara.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya mashabiki wa timu hiyo kulalamikia kiwango kibovu licha ya kupata ushindi kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Kagera Sugar.

Kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar ambao ulikuwa ni wa ufunguzi kwa msimu wa 2021/22 Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo mzawa,Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwa shuti kali ndani ya 18 Uwanja wa Kaitaba.

Nyota huyo alisema kuwa kwenye mechi yao dhidi ya Kagera Sugar walicheza wakiwa wamechoka baada ya kutumia nguvu mbele ya Simba lakini wana imani ya kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zijazo.

"Mchezo wetu dhidi ya Kagera ulikuwa mgumu,lakini licha ya ugumu tunashukuru kuanza ligi vizuri kwa ushindi ambao umetuongezea nguvu katika michezo ijayo.

“Mchezo wa mwanzo tulicheza chini ya kiwango kutokana na miili kuchoka kwa kuwa tulitoka kwenye mchezo mgumu dhidi ya Simba hivyo tunaamini kwamba kwa mechi zijazo tutafanya vizuri na kupata matokeo chanya,hata safari ile ya Kagera Sugar nayo iliweza kutufanya tuwe wachovu, kwa mechi zijazo ni kazikazi," .

Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ina pointi sita kwa kuwa mchezo wake wa pili ilishinda pia bao 1-0 dhidi ya Geita Gold, Uwanja wa Mkapa, mchezo wao ujao ni dhidi ya KMC, Uwanja wa Majimaji, Songea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live