Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho asababisha kiungo huyu kugoma kusaini Yanga

Kagoma Auchoo.jpeg Aucho asababisha kiungo huyu kugoma kusaini Yanga

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeelezwa kuwa kiungo mkabajai wa Singida Fountain Gate, Yusuf Kagoma amekataa kusaini mkataba  Yanga kutokana na ushindani wa namba ambao upo katika kikosi hicho.   Kagoma ni kati ya wachezaji waliokuwepo katika mazungumzo na  Yanga, kabla ya kuchukua maamuzi ya kwenda  Simba ambayo yupo katika hatua za mwisho za kumwaga wino.   Kiungo huyo ambaye aliitwa katika kikosi cha Timu ya taifa, Taifa Stars  kilichoifunga Zambia bao 1-0 ugenini katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia kama angetua Yanga basi angekutana na ushindani kutoka kwa Mganda Khalid Aucho, Jonas Mkude na Zawadi Mauya wanaocheza nafasi ya kiungo mkabaji.   Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Yanga, kiungo amekataa kusaini mkataba huo kutokana na ushindani wa namba uliokuwepo katika timu hiyo ambayo imepanga pia kuongeza mchezaji mwengine wa kigeni anayecheza nafasi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live