Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho apewa kocha 'mkorofi'

Khali Aucho Kh Khalid Aucho

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mtata, Paul Put ndiye ataiongoza timu ya taifa ya Uganda ambayo nahodha wake ni nyota wa Yanga, Khalid Aucho baada ya jana kutambulishwa rasmi na FUFA jijini Kampala, Uganda.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 67, anajiunga na Uganda kuchukua nafasi iliyoachwa na kocha Milutin Sredojevic 'Micho' aliyetimuliwa mwezi Septemba.

Put ambaye ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika akiwa amewahi kuzifundisha timu kadhaa za taifa na klabu, anasifika kwa ukali na kusimamia vyema misimamo yake jambo ambalo hupelekea kuvunjika mara kwa mara kwa mikataba yake.

Mfano ni mwaka 2018 ambapo kocha huyo aliamua kuvunja mkataba wa kuinoa timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars' kwa kile kilichodaiwa ni kutofurahishwa na mazingira ya kazi yake.

Ni kocha mwenye uzoefu wa soka la Afrika na amepata mafanikio kadhaa mojawapo ikiwa ni kuifikisha Burkina Faso katika Fainali ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2013.

Amewahi kuziongoza pia Congo, Gambia na Guinea huku akiwahi pia kuifundisha USM Alger ya Algeria

Chanzo: Mwanaspoti