Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho anaendelea freshi

Khali Aucho Kh Aucho anaendelea freshi

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa kimataifa wa Yanga, Khalidi Aucho raia wa Uganda aliyepata majeraha juzi dhidi ya Mtibwa Sugar, anaendelea vizuri kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo, Shecky Mngazija ambaye amesema anaweza kutumika hata wikiendi ijayo.

“Aucho amepata majeraha ya kawaida tu kwenye mchezo huo mguu ulishtuka tukaona tusiendelee kumuacha uwanjani kwasababu angeweza kupata majeraha makubwa zaidi, ndipo mwalimu akaona ambadilishe kwa ajili ya mapumziko.”

“Licha ya kupata jeraha hilo mpaka muda huu tunaozungumza Aucho anaendelea vizuri na analeta matumaini makubwa sana na mashabiki wasiwe na wasiwasi na kiungo huyo,” amesema Shecky Mngazija.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live