Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho amejijengea ufalme wake pale Jangwani

Aucho9175 Aucho amejijengea ufalme wake pale Jangwani

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Al Ahly ya pale nchini Misri imeshaletewa zaidi ya ofa 3 za kumuhitaji kiungo wao wa chini kutoka Mali, Aliou Dieng, lakini ofa zote walizipiga chini.

Sababu kuu ikiwa ni kukosa mbadala sahihi wakuweza kudundika na midundo yake pale katikati mwa kiwanja. Ahly wamekuwa wakimtegemea sana Aliou Dieng katika nafasi ya kiungo kwa takriban misimu 4-5 sasa.

Sio kwamba fedha hawazihtaji, lakini perfect replacement bado iliwapa changamoto sana. Ndiyo maana kwa sasa wamekuwa wakijaribu kuwatumia Nabil Koka na Marwan ili kuona kama watatundika vyema lakini bado wakaona kuna haja yakuendelea kuwa na Dieng.

Huko ni kwa upande wa Al Ahly lakini kwenye ardhi ya Mwalimu Nyerere, kuna kiungo Khalid Aucho anayekipiga kunako Klabu ya Yanga Sc, huyu bwana ile mido kajimilikisha na wananchi wamekuwa kwa muda mrefu wanatafuta taratibu mbadala wake lakini bado Hawajapata perfect replacement.

Ndiyo maana ukigusia kuhusu kuuzwa kwa Aucho, sio viongozi wala mashabiki wa Yanga Sc wanaweza wakakuelewa hata siku moja.

Aucho amekuwa mhimili kwenye kikosi chake kiasi kwamba ukiitazama Yanga Sc bila Aucho. Yanga ya Aucho basi unaona kabisa kwa nini wanamuhtaji kila mechi awe fit asilimia 100.

Kuwa na mchezaji bora ni jambo moja lakini kutafuta back up nzuri huwa ni shughuli kubwa sana bila kufanya uchunguzi vizuri unaweza ukajikuta unasajili na kuondoa kila dirisha.

The Tank amejimegemea kieneo chake katika midfield ya Yanga Sc tangu ajiunge na Klabu hiyo. He Goes By the Name Khalid Aucho "The Tank" "Doctor of Football".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live