Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho alitakiwa nyekundu, Ajibu njano

Ajibu Auchooo Aucho alitakiwa nyekundu, Ajibu njano

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo kati ya Coastal Union na Yanga jana katika dimba la Mkwakwani, Ibrahim Ajibu alistahili kupigwa kadi ya njano na Khalid Aucho alistahili kadi nyekundu.

Mwamuzi Emmanuel Mwandembwa ndio kwanza karejea kwenye ligi, kashindwa kufanya uamuzi sahihi kwenye jambo la wazi.

Mwamuzi aliona ndiyo maana alitoa kadi ya njano kwa Aucho, asingekuwa ameona ingekuwa jambo jingine lakini kama aliona na akashindwa kufanya maamuzi sahihi maana yake alishindwa kutafsiri sheria.

Yanga wanapaswa kulifanyia kazi jambo hili maana kuna siku Aucho atapata kadi nyekundu au kusimamishwa na kuwapa mizigo.

Aucho ni mchezaji professional na mkongwe, hapaswi kuingia kwenye mitego hii kirahisi na anapaswa kuifikiria timu zai yake yeye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live